Back to top

Fedha za UVIKO 19 zamoto, Ndalichako atoa maagizo kwa watendaji.

24 October 2021
Share

Waziri wa Elimu, Prof.Joyce Ndalichako amewaagiza watendaji wa wizara na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo zitakazotekeleza miradi ya fedha za UVIKO 19, Shilingi Bilioni 64.9 kuhakikisha hadi kufikia tarehe 30 mwezi huu wawe wamekamilisha mpango wa namna watakavyotekeleza miradi hiyo.
.
Waziri Ndalichako pia amewonya watendaji kuzingatia bei halisi za vifaa vitakavyo tumika katika miradi.
.
Ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza Jijini Dodoma wa kati akitoa mchanganuo wa fedha zitakazotekeleza miradi hiyo.
.
Waziri Ndalichako amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof.Leonard Akwilapo aandae mfumo wa uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa  miradi utakao wezesha kubaini matatizo yatakayojitokeza na kuyatatua kwa wakati.