
Baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kukutana, chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho Mh. Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Jijini Dodoma, Kamati hiyo pamoja na mambo mengine imeazimia kuwaita wanachama na Viongozi wake watatu ambao ni Mh. Jerry W. Slaa(MB), Mh.Josephat M. Gwajima(MB) na Mh.Humphrey Polepole(MB) ili kuwapa nafasi ya kuwasikiliza kama inavyoagizwa na Kanuni za Uongozi na Maadili.
