
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imekubali kupokea maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu Mohamed Ling'wenya katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake, na kutupilia mbali hoja zote saba za pingamizi la upande wa utetezi kwa kukosa mashiko ambao walikuwa wakiiomba mahakama kutopokea kielelezo hicho.
Kutokana na uamuzi huo uliotolewa na Jaji Joachim Tiganga katika shauri dogo ndani ya kesi ya msingi ya uhujumu uchumi, mahakama sasa itaendelea kusikiliza kesi ya msingi kwa shahidi wa Jamhuri SP Jumanne Malangahe kuendelea kutoa ushahidi wake mahakamani.
