
Kufuatia kusambaa kwa taarifa kuhusu baadhi ya wagonjwa kutohudumiwa ipasavyo na wahudumu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala iliyopo Jijini Dar es Salaam, Wizara ya Afya imeyaelekeza mabaraza ya kitaaluma kufika katika hospitali hiyo kwa ajiri ya kufanya ufuatiliaji ili kubaini ukweli juu ya taarifa hizo kisha kuchukua hatua stahiki.
