Back to top

Idadi ya maambukizi ya COVID-19 nchini Uganda.

14 May 2020
Share

Taarifa ya Wizara ya afya nchini uganda kwa vyombo vya habari inaashiria maambukizi mapya 13 ya kirusi cha Corona na kuifikisha idadi ya visa kuwa 139.

13 hao wote ni madereva,7 wa uganda,5 kutoka Kenya huku 1 kutoka Eritrea aliyepitia Sudan Kusini,Kenya,Tanzania na kisha Uganda kupitia mpaka wa Mtukula.

Takribani sampuli 2,104 zimefanyiwa vipimo,miongoni mwazo 1741 zikiwa za madereva huku 363 kutoka maeneo tofauti ya ndani mwa Uganda.