Back to top

Idadi ya vifo vitokanavyo na Corona yafikia 14,757 ulimwenguni.

23 March 2020
Share

Idadi ya maambukizi na vifo vinavyotokana na virusi vya Corona imeongezeka duniani, hadi sasa watu 341,816 wameambukizwa huku zaidi ya 14,757 wakifariki dunia.

Nchini Italia takriban watu 60,000 wamepata maambukizi huku idadi ya vifo ikikaribia 5500.

Nchini Uhispania, serikali imetangaza kurefusha muda wa hali ya dharura kuanzia leo baada ya idadi ya vifo na maambukizi kuongezekaNchini Misri, Rais Abdel-Fattah el Sissi amewahimiza raia wake kusaidia kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo kwa kubakia nyumbani na kuepuka kukaribiana wakati nchi hiyo ikithibitisha visa 327 vya maambukizi na vifo 15. 

Wakati huo huo, mashirika ya ndege ya Emirates na Turkish Airlines yamesitisha safari zake za kimataifa kutokana na mripuko huo wa virusi vya Corona.