
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo ametoa siku 45 kwa wataalamu wanaojenga miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kukamilisha miradi hiyo ikiwemo ya uchimbaji visima na ujenzi wa majosho bila kukwama ili isaidie kuimarisha mfumo wa ikolojia vijijini.
