Back to top

Jaji Kesi ya Mbowe ajitoa, atoa sababu.

20 October 2021
Share

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi katika kesi inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Bwana Freema Mbowe na wenzake watatu.
.
Aidha, imekubali kupokea maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili Adam Kaswekwa maarufu 'ADAMOO' kama kielelezo cha kwanza ambayo upande wa utetezi katika pingamizi lake ulitaka mahakama isipokee kwa kwa madai yalichukuliwa kinyume na sheria.
.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Kiongozi Mhe.Mustapha Siyani ambaye amesema mapingamizi hayo yamekosa mashiko, hivyo na kwa uamuzi huo kesi ya msingi itaendelea.
.
Wakati huo huo Jaji Mustapha Siyani amejitoa kusikiliza kesi hiyo kutokana na kile alichokieleza majukumu mapya aliyonayo ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo yanambana kusikiliza kesi hiyo mfululizo kama inavyotakiwa.
.
Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi No.16 ya mwaka 2021 yenye mashtaka yakiwemo ya ugaidi washtakiwa ni Halfani Bwire Hassan, Adam Kusekwa, Mohamed Ling'wenya na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.