Jeshi la Ethiopia Jumapili lilizindua mashambulizi mawili ya anga katika sehemu muhimu zinazoshikiliwa na Tigray.
Mashambulizi yanafanyika mbali ya mji mkuu wa Mekele, na kutoa ishara kwamba kuna uwezekano wa jeshi kusambaza kampeni ya mashambulizi ya anga.
Mpaka sasa mashambulizi yamepingwa na Jumuiya ya Kimataifa, na kusimamisha safari za ndege za Umoja wa Mataifa kwenye sehemu yenye tishio la baa la njaa.
Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Selamawit Kassa, amesema kwamba Jumapili eneo la Magharibi la Mai Sebri ambalo lilitumika kama kambi ya mafunzo ya TPLF, na komandi yao ya kijeshi lililengwa na shambulizi la anga.
