Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa A. Musssa amesema Jeshi la Polisi litaendelea kujikita katika kuandaa mipango mbalimbali ili kutatua changamoto walizonazo wananchi ikiwemo makosa yanayotokana na ukatili wa kijinsia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa A. Musssa wakati akifungua mkutano wa tatu wa Makamishna na Makamanda wa Polisi wa Mikoa Tanzania katika kuimarisha upatikanaji wa haki jinai kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.
