Back to top

JPM aagiza aliyepuuza maagizo ya Lugola kusimamishwa kazi.

06 October 2019
Share

Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli amesikitishwa na kitendo cha polisi kupuuza maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.   Kangi Lugola aliyoya toa hivi karibuni, kuwataka askari tisa kuhamishwa kituo Wilayani Laela Mkoani Rukwa wanaotuhumiwa kuwanyanyasa wananchi na kuwabambikizia kesi.

Rais Magufuli amelazimika kumpigia simu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro na kumtaka amsimamishe kazi Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Polycarp Urio.

Rais Magufuli amechuku hatua hiyo Mjini Laela Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa alipokuwa akizindua barabara ya kiwango cha lami ya Tunduma - Sumbawanga, yenye urefu wa Kilomita zaidi ya 223 na kugharimu Shilingi Bilioni 375 .

Amewataka wananchi wa mikoa ya Songwe na Rukwa kutohujumu miundombinu na badala yake wawekeze kwenye viwanda ili kunufaika na fursa za uchumi kupitia Usafirishaji.