Back to top

Kasulu yatakiwa kudhibiti uhalifu

20 July 2018
Share

Serikali ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imeombwa kuongeza kasi ya udhibiti wa vitendo vya uhalifu na utekaji magari barabarani kutokana na vitendo hivyo kuathiri shughuli za wananchi ambao wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo kutokana na kuwepo kwa matukio ya uhalifu.

Wamesema kumekuwa na kulegalega kwa udhibiti wa wahalifu na kusababisha kuongezeka kwa matukio ya wizi na uhalifu wa aina mbalimbali hali ambayo isipodhibitiwa mapema itasababisha wananchi kushindwa kushirikia shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Kasulu Titus Mguha amesema katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Kasulu kuwa serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kuwa na nyumba kumi za kiusalama, mpango ambao umeanza kusaidia kupunguza uhalifu katika wilaya hiyo huku mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Fatma Hussein akiwataka watendaji kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro.