Back to top

Katibu wa Mbunge ahojiwa mauaji ya watu 6 Geita.

15 November 2021
Share

Baada ya Mbunge wa Jimbo la Mbogwe mkoani Geita Mh. Nicodemas Maganga kutoa madai bungeni Dodoma juu ya wananchi sita akiwemo binamu yake kuuawa, Jeshi la Polisi mkoani humo limewahoji watu nane akiwemo Katibu wa mbunge huyo, huku likimtaka Mbunge huyo kutoa ushirikiano ili kuthibitisha ukweli wa madai hayo.