Back to top

Kenya yaondoa na kupunguza marufuku zilizowekwa kudhibiti Covid-19.

01 May 2021
Share

Rais Uhuru Kenyatta ameondoa marufuku ya usafiri iliyowekewa kaunti tano za Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru baada ya maambukizi ya Covid-19 kutangazwa kupungua katika kaunti hizo.

Akiongoza taifa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi katika Ikulu ya Nairobi Rais Kenyatta  pia ametangaza kurejea kwa ibada za ana kwa ana katika kaunti hizo tano ambapo sehemu za ibada zimetakiwa kuhakikisha zinazingatia kikamilifu masharti ya kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Huduma za mahoteli na mikahawa katika kaunti hizo tano ambazo zilikuwa zimesitishwa pia zitarejeshwa ,huduma za  mabaa zitaruhusiwa ila zitahitajika kutoa huduma hadi saa moja usiku.

Kiongozi wa taifa alisema serikali itakuchukua kila hatua kuhakikisha usalama wa wakenya huku akitoa wito kwa kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya Covid-19.

Hata hivyo rais kenyatta  amesema kuwa marufuku dhidi ya mikutano ya kisiasa itaendelea.

Kwa mujibu wa Wizara ya elimu, shule zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 10 mwezi Mei.