Back to top

KENYATTA, KAGAME WAKUBALIANA JUU YA M23

19 November 2022
Share

Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Rwanda Paul Kagame, wamekubaliana juu ya haja ya waasi wa M23 kusitisha mapigano na kujiondoa katika maeneo ya Mashariki mwa Congo.

Taarifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, imesema Rais Kagame pia amekubali kumsaidia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, kuwahimiza waasi wa M23 kutekeleza matakwa hayo.

Mbinu za kufanikisha azma hiyo zitajadiliwa wakati wa duru ya pili ya mazungumzo katika mji mkuu wa Angola Luanda juma lijalo.

Naibu msemaji wa Rais wa Congo, amesema hatua hiyo inatia moyo kuona Rais Paul Kagame, ametambua kuwa anaweza kuwashawishi waasi wa M23, lakini amesema Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inasubiri kuona kitakachotokea katika uwanja wa vita.

Mapigano ya hivi karibuni kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.