
Shahidi wa 5 katika kesi ya Uhujumu Uchumi na Vitendo vya Kigaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Shahidi huyo wa 5 upande wa Jamhuri, Bw.Fredy Kapala ambaye ni Mwanasheria wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania anatoa ushahidi wake akihojiwa na wakili mwandamizi wa serikali Nassoro Katuga.
Kesi hii inasikilizwa na Jaji Joachim Tiganga ambapo upande wa Jamhuri umedai unamashahidi 24 katika kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021ya Uhujumu Uchumi yenye Mashtaka Sita.
