
Shahidi wa Pili katika Kesi ndogo inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe na wenzake watatu, askari mpelelezi Ricado Msemwa, ambaye ni shahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu, Mohammed Abdillah Ling'wenya, katika kesi ya uhujumu uchumi, ameanza kutoa ushahidi wake mahakamani hapo.
