
Shahidi wa kwanza Kamanda wa Polisi wa Kinondoni ACP Ramadhani Kingai anaendelea kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi na vitendo vya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe na wenzake watatu na sasa anahojiwa maswali ya dodoso kutoka kwa upande wa mawakili wa serikali akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Robart Kidando na kuendelea kuibua kwa mvutano kutokana upande wa mawakili wa utetezi kupinga baadhi ya ushahidi unaotolewa ikiwemo mkanganyiko wa tarehe za kukamatwa watuhumiwa kwa mikoa tofauti kati ya Dar es salaam Morogoro na Moshi.
Kesi hiyo yenye mashahidi 24 inasikilizwa na Jaji Joachim Tiganga katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa Sinza jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Bwire, Kasekwa, Ling'wenya na Mbowe ambao wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya kula njama kufanya vitendo vya kigaidi, ikiwemo kulipua vituo vya mafuta na kumdhuru Sabaya kesi hiyo inaendelea mpaka sasa.
