Back to top

Kesi ya vigogo 9 CHADEMA inaendelea kunguruma Kisutu.

11 September 2019
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu jijini Dar es Salaam inaendelea kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Mhe.Freeman Mbowe ambapo shahidi wa nane anatoa ushahidi wake kwa sasa.

Shahidi huyo Bernard Nyambari mkuu wa upelelezi wilaya ya kipolisi mbagala upande wa jamhuri anaendelea kutoa ushahidi wake akiongozwa na wakili mkuu wa serikali Dokta.Zainab Mango.

Hakimu anayesikiza kesi hiyo Thomas Simba anaendelea na kesi hiyo huku washtakiwa wote tisa wakitetewa na wakili Msomi Peter Kibatala na kesi hiyo inaendelea mpaka sasa.

Washtakiwa wote tisa wapo mahakamani na upande wa jamhuri unaendelea kuwasilisha ushahidi hapa Kisutu.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 13 ya kula njama ya kufanya mkusanyiko usio halali kati la Februari 1 Mpaka 16 mwaka 2018.