Back to top

Lukuvi akagua mpaka wa Tanzania na Kenya.

22 December 2021
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekagua uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya Tanzania na Kenya katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara na kupongeza wapima wa nchi hizo mbili kwa kufanikisha kuweka alama 205.

Aidha, Waziri Lukuvi aliwashukuru marais wa Tanzania na Kenya kwa kukubaliana kuendelea na kazi ya uimarishaji mpaka huo wa kimataifa kwenye eneo la hifadhi ya Taifa ya Mbuga ya Serengeti na Masai Mara kwa upande wa Kenya ambapo uimarishaji wake ulisimama kwa muda.