
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi amesema serikali imeamua kuweka muongozo wa kusimamia shughuli za udalali nchini ikiwemo kuwatambua madalali ,kuweka utaratibu na kudhibiti kazi zao pamoja na kutoa cheti na kitambulisho kwa wanaofanya shughuli hizo.
Aidha Waziri Lukuvi amesema kutakuwepo na utambulisho wa nyumba zinazopangishwa sambamba na ulipaji wa kodi kwa wenye nyumba na madalali pindi wanapofanya upangishaji.
