Back to top

Maambukizi ya VVU yaongezeka mkoani Shinyanga.

02 December 2021
Share

Maambukizi ya virusi vya UKIMWI mkoani Shinyanga yameongezeka kutoka asilimia 3.9 mwaka jana hadi kufikia asilimia 4.7 huku watu zaidi ya 6,000 kati ya maelfu waliopima wakibainika kuwa na maambukizi mapya ya VVU, hali iliyopelekea kuufanya mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa maambukizi ya VVU.
.
Takwimu hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani huku mila potofu, ndoa za mitala, ulevi, ngono zembe na wanaume kutofanyiwa tohara vikitajwa kuwa ni miongoni mwa visababishi vya ongezeko la maambukizi.