Back to top

Madarasa 2 na ofisi ya Kata zaanguka kutokana na mvua Ruvuma.

25 March 2020
Share

Mvua zinazoendelea kunyesha zimeangusha jengo la madarasa mawili yanayojengwa kwa nguvu za wananchi katika shule ya msingi mitendewawa na pia kuangusha ofisi ya kata ya Seedfarm Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
  
Mwenyekiti wa mtaa wa Mitendewawa Bw.Aron Mhagama anasema kuwa jengo hilo lilifikia hatua ya linta Agosti mwaka jana na kwa utaratibu katika hatua lilipofikia ilitakiwa halmashauri waliezeke.
 
Mwenyekiti wa kamati za huduma za uchumi wa manispaa ya songea Bw.Festo mlelwa  amesema kuwa watalifikisha suala hilo kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya songea ili liweze kufanyiwa kazi.