Madereva Dangote waomba viongozi wa kitaifa kuingilia kati mgomo wao.

Mgomo wa madereva wa kiwanda cha saruji cha  Dangote zaidi ya mianne umefikia siku ya kumi sasa, huku serikali ya mkoa ikigonga mwamba licha ya kufanya vikao vitatu ili kupata suluhu  ya changamoto  zinazowakabili ikiwemo maslahi bora ya kazi na hivyo kuomba viongozi wa kitaifa  kuingilia  kati  huku  hitaji  lao kubwa  likiwa ni  kuwaondoa mawakala wa usafirishaji ili kiwanda kiajiri madereva moja kwa moja.
.
Kauli hiyo wameitoa mara baada ya kumaliza kikao na mkuu wa mkoa na kusisitiza kuendeleza mgomo licha ya baadhi ya changamoto kupatiwa  ufumbuzi.