Back to top

UTAFITI UMEWEZESHA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA.

28 April 2024
Share

Wizara ya Kilimo imebainisha kuwa utafiti unaofanywa, umeendelea kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora za mazao, zenye sifa za kustahimili mabadiliko ya tabia nchi, magonjwa na wadudu waharibifu pamoja na kuongeza  kiwango cha mavuno.

Hayo yamebainishwa zikiwa zimebaki siku 3, kuelekea kusomwa kwa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, ambapo imesema suala la afya ya udongo ni muhimu katika kilimo, hivyo tafiti zimekuwa zikifanyika kuhakikisha mkulima analima kwa tija .

Miongoni mwa matokeo ya utafiti,  ni utafiti uliobaini uchachu katika udongo, na Watafiti wanashauri matumizi ya chokaa kwa kuzingatia hali ya eneo husika, kutokana kiwango cha athari iliyopo. 

Wizara imeeleza kuwa Matumizi ya viuatilifu na pembejeo za mbolea ni muhimu, lakini kwa kuzingatia kiwango maalumu ambapo Watafiti wameendelea kutafiti na kushauri viwango maalumu vya mbolea vinavyofaa kutumiwa katika mazao na mbegu husika katika maeneo waliopo. 

Kwa upande wa uongezeaji thamani mazao, utafiti umesaidia kupunguza hasara anayopata mkulima, na hatimaye kumuongezea tija mfano zao la zabibu sio tu kutafuna bali inatumika pia kutengeneza bidhaa zingine, ikiwemo mvinyo, zabibu za mezani na viungo.