Back to top

Madiwani walalamika Stendi ya Mabasi kukosa Maji Mbinga.

02 May 2018
Share

Madiwani wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma wamelalamikia kituo kikuu cha mabasi cha Mbinga kukosa maji kutokana na mifumo mibovu ya miundombinu ya maji hali inayosababisha abiria kujisaidia kwenye nyumba za jirani na kituo hicho.

Kutokana na kukosekana kwa maji katika kituo hicho mabasi cha Mbinga Madiwani wametaka kero hiyo ishughulikiwe  ili kuwaondolea adha abiria na wananchi kwa ujumla ambao wanalazimika kujisaidia kwenye nyumba za jirani na kituo hicho.
Kaimu mhandisi wa maji halmashauri ya mji wa Mbinga Mhandisi Ntelezu Masanja anaeleza namna alivyoshughulikia kero hiyo.

Kwa  upande  wake kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mbinga Bw.Kevin Mapunda anaagiza kutatuliwa kwa kero hiyo haraka.