Back to top

Majambazi watano wauawa na Polisi, Kagera.

31 December 2021
Share

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewaua watu watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha mbalimbali za kivita ambapo Jeshi hilo limesema majambazi hao walikuwa wakijiandaa kuteka magari ambayo yanapita kwenye barabara kuu inayounganisha mkoa huo na nchi jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC).