Back to top

Majeruhi 6 wa ajali ya Moto Morogoro wafariki.

14 August 2019
Share

Majeruhi wengine sita wa ajali ya moto iliyotokea eneo la Msavu mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki, wamefariki wakati wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimhimbili.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha, ametoa taarifa hizo leo kwa waandishi wa habari na kuwema kuwa maiti zote zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti wakati wakisubiri taratibu nyingine.

Aligaesha ameongeza kuwa wagonjwa 17 akiwamo mtoto mmoja, hali zao ni mbaya na wapo katika chumba maalum cha uangalizi (ICU).

Amesema kwa sasa katika hospitali ya Muhimbili wamebaki na majerhi 32 ambao wanaendelea kuwapatia matibabu.