Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa zimeendelea kusababisha adha kwa wananchi baada ya kusababisha vifo vya watu wawili na nyumba saba kubomoka katika wilaya ya Kalambo na huku ikisababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya Kasisiwe katika manispaa ya Sumbawanga na kupelekea mama mjamzito kujifungulia vichakani baada ya mto kujaa maji.
Meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) mkoani Rukwa Eng. Seth Mwakyembe , amesema, serikali imejipanga kufanya marekebisho ya madaraja yote ikiwemo daraja la kasisiwe huku mkuu wa wilaya ya kalambo julieth binyura akiwataka wananchi kutovuka kwenye mito iliyojaa maji.