Back to top

Mamilioni ya watu Afrika Mashariki hatarini, Corona, Nzige na mafuriko

22 May 2020
Share

Benki ya Dunia imeonya kuwa maisha ya mamilioni ya watu katika Afrika Mashariki yamo hatarini kutokana na majanga ya virusi vya Corona, Nzige na mafuriko.

Ili kupunguza athari za majanga hayo, Benki hiyo imetenga dola milioni mia tano kwa ajili ya nchi zilizoathirika na janga la Nzige hao wa jangwani.

Wimbi jipya na kubwa zaidi la wadudu hao linatarajiwa kuvamia eneo la Afrika Mashariki ambalo halijawahi kushuhudia idadi kubwa ya wadudu hao kwa miaka 70.

Mabadiliko ya tabianchi yanatajwa kuwa ni mojawapo ya sababu za kujitokeza kwa wadudu hao.

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba uvamizi huo wa nzige kwa sasa ni mbaya zaidi nchini Kenya, Somalia na Ethiopia.

Aidha mbali na barani Afrika janga hilo la nzige pia limevamia kusini mwa Iran na sehemu za Pakistan.