Back to top

Matapeli wawachezea mchezo mchafu wakulima Ruvuma.

05 November 2019
Share

Wakulima zaidi ya 50  katika kijiji cha Namatuhi wilayani Songea mkoani Ruvuma wametapeliwa mahindi yao yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 na matapeli ambao wamechukua mahindi yao bila kuwalipa fedha zao na kusababisha waishi maisha magumu.
 
Wakulima hao wanasema kuwa watu waliochukua mahindi yao ni Bw.Wiligis Choma na Bruno Ng'oma kupitia kampuni yao ya Kaunga Flety Limited mwaka jana na hivyo msimu wa 2019 watashindwa kuingia shambani kutokana na kukosa fedha za pembejeo baada ya kutapeliwa fedha zao za mahindi.
 
ITV imemtafuta Bw. Wiligis Choma aliyedai Bw. Bruno Ng'oma alifariki machi 5 mwaka 2018 na kwamba biashara ya mazao aliifanya yeye binafsi huku wakulima wakitilia shaka kwamba Bw. Ng'oma alikufa kwakuwa hawakuruhusiwa kuuona mwili kwa madai uliharibika.
 
Kwa upande wake Bw.John Wella ambaye aliuziwa mahindi anasema kuwa fedha zote waliwalipa Bw.Bruno Ng'oma na Wiligis Choma baada ya kuletewa mahindi ya wakulima huku mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Pololet Mgema akisema wote waliowatapeli wakulima watachukuliwa hatua za kisheria.