Back to top

Mbaroni kwa kuwatapeli wanaokaribia kustaafu.

18 December 2021
Share

Watu watano wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera baada ya kuwatapeli kwa njia ya mtandao wa mawasiliano ya simu watumishi wa serikali wanaokaribia kustaafu kwa kujitambulisha kuwa wao ni watumishi wa ofisi ya Hazina makao makuu wanaoshughulikia mafao ya wastaafu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadh Juma Haji amesema kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakiwapigia simu watumishi hao na kuwaomba pesa kwa kile walichokuwa wakidai wangewaharakishia upatikanaji wamafao yao.