Back to top

MFUMO TIBA SHIRIKISHI KUKABILI MALARIA WAIVA.

19 November 2021
Share

Mawaziri wa Serikali za Baadhi ya Nchi za Maziwa Makuu za Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanaoshughulikia masuala ya afya ambao jana wamekutana nchini Rwanda kujadili namna ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto,  wamekubaliana kuweka mfumo wa tiba shirikishi wa kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kutoka nchi moja kwenda nyingine.
.
Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Godwin Mollel aliyezungumza na waandishi wa habari akiwa mkoani Kagera baada ya kukutana na maofisa wa idara ya afya wa hospitali ya rufaa ya mkoa huo.