
Naibu Waziri Wizara ya Afya Dkt. Godwin Mollel ameyaagiza mabaraza yote ya kitaaluma kwenye sekta hiyo, kuhakikisha watendaji wake wanapita mara kwa mara kukagua mienendo na utendaji kazi wa watumishi kwenye vituo vyao.
Dkt. Mollel ameyasema hayo alipokuwa kwenye ziara ya kawaida ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala na kuzungumza na watumishi ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa ya baadhi ya wananchi kudai kutokuhudumiwa vema hospitalini hapo.
