Back to top

Miili 64 yakutwa kwenye kontena Msumbiji.

24 March 2020
Share

Miili 64 inayodhaniwa kuwa ni ya wahamiaji kutoka nchini Ethiopia yakutwa katika kontena la lori nchini Msumbiji huku wengine 14 wakikutwa wako hai,Maafisa uhamiaji nchini humo wamethibitisha.

Uchunguzi unaendelea licha ya watu hao ambao walitokea nchini Malawi kudaiwa wamekufa kwa kukosa hewa.

Maafisa uhamiaji wamesema wakati wakijaribu kusimamisha lori hilo dereva alionyesha dalili ya kusita na walisikia kama sauti ya watu wakigonga kontena.