Back to top

Mitambo ya kutengenezea fedha yakamatwa Rukwa.

24 December 2021
Share

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limewakamata  watu wawili wakazi wa mtaa wa Bangwe Manispaa ya Sumbawanga  wakiwa na mitambo ya kutengenezea fedha pamoja na fedha za noti bandia  kiasi cha  shilingi  millioni tatu na laki sita huku kati ya hizo noti za elfu kumi zikiwa 420, noti za elfu tano 143 na noti za elfu mbili  zikiwa 50.