
Serikali imeweka mikakati thabiti kukabiliana na sumu kuvu zitokanazo na mazao hasa Mahindi na Karanga ili kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa kwa kujenga maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi wa sumu hiyo ili afya za wananchi ziwe bora na salama.
Hayo yameelezwa mjini Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa sera kutoka Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kuhusu utekelezaji wa malengo ya milenia.
Bwana Mibavu amesema katika kutekeleza malengo hayo ya milenia serikali imedhamiria kuondokana na sumu kuvu kwa kufanya ujenzi wa kisasa wa maabara hiyo ya kisasa itayotumia vifaa vya kisasa kulingana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.
Afisa mkuu wa utafiti kutoka wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na uvuvi Zanzibar Juma Omary Abdallah amesema mipango waliyojiwekea kuhakikisha usalama wa chakula kwa wannachi unakewepo muda wote kuanzia maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake afisa mwandamizi wa programu ya kilimo endelevu kutoka shirika la kimataifa la chakula duniani (FAO) Ola Mollar, amesema shabaha ya FAO ni kuongeza uelewa wa utatuzi wa changamoto mbalimb ali za kilimo zilizopo katika sekta ya kilimo katika nchi mbalimbali barani afrika ikiwemo Tanzania.
