
Watu 6 wamethibitika kufariki dunia wawili kati yao wakiwa maafisa polisi, kufuatia milipuko miwili kutokea jijini Kampala nchini Uganda karibu na Bunge na kituo cha Polisi katikati mwa jiji, huku watu 33 wakijeruhiwa na uhakiki wa waliojeruhiwa ukiendelea kufanyika ili kujua idadi yao.
.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa bomu jingine limekutwa karibu na Transifoma katika jengo la Kooki Tower na mengine mawili yamekutwa karibu na barabra ya Buganda ambapo yote yalitenguliwa huku Kitengo cha Polisi cha kupambana na ugaidi kikiendelea kutafuta mabomu mengine zaidi kama yapo ili kuyategua.
