Back to top

MOTO WATEKETEZA VIBANDA 43 VYA WANFANYABIASHARA SONGWE.

16 November 2021
Share

Vibanda 43 vya Wafanyabiashara katika soko la Manzese la mjini Tunduma mkoani Songwe vimeteketea kwa moto.
.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bwana Omary Mgumba amesema moto huo ulioanza saa kumi alfajiri haukusababisha madhara kwa binadamu.
.
Amesema wakati moto huo unaanza hapakuwa na magari ya zimamoto kwenye mji huo.
.
Amesema kuna magari mawili tu yanayotegemewa kwa ajili ya shughuli kama hiyo na moja lilikuwa Mbeya kwa ajili ya matengenezo na linguine lilikuw aeneo la Mbozi.
.
Mkuu huyo wa mkoa ambaye ameunda tume ya kuchunguza chanzo cha moto huo, amesema umedhibitiwa kwa ushirikiano wa wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani Songwe.