Back to top

Msafara wa Waziri Biteko wapata ajali waandishi 4 wajeruhiwa Kagera.

03 July 2020
Share

Waandishi wanne wa habari kutoka mkoani Geita wamenusurika kifo baada ya moja ya gari katika msafara wa Waziri wa Madini kupinduka na kutumbukia mtaroni katika kijiji cha Mrusagamba wilaya ya Ngara mkoani mkoani Kagera.

Kamanda wa polisi wilaya ya Ngara Mrakibu Mwandamizi wa polisi Abeid Maige amethibitisha ambapo amaewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo  Nizareti Ndekia TBC 1,Salma Mrisho Star TV, Emanuel Ibrahimu Clouds TV na Victor Bariety channel Ten.