Back to top

MSIWASHAMBULIE ASKARI WETU - JESHI LA POLISI

17 September 2023
Share

Jeshi la Polisi nchini limewataka watu wenye tabia ya kuwashambulia Askari wa Jeshi hilo, ambao wanakuwa wamebeba silaha kuacha tabia hiyo kwani, Askari wanapotekeleza majukumu yao wameruhusiwa na sheria kubeba silaha ili waweze kulinda maisha ya watu, mali zao, maisha yao na mali ya serikali ikiwemo silaha husika.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo katika mitandao yake ya kijamii, limesema Askari naye ni binadamu kama binadamu mwingine na sheria inamruhusu kutumia silaha hiyo kulinda uhai wake, uhai wa mtu mwingine na mali za huyo mtu.