Back to top

Mtoto afariki kwa ajali ya treni Tanga.

16 January 2022
Share

Shirika la Reli Tanzania(TRC) limetoa taarifa kwa umma kuwa Treni yake ya abiria yenye injini namba 9022 imepata ajali majira ya saa 10 alfajiri kati ya Mkalamo na Mvave wilayani Pangani mkoani Tanga ambapo behewa 5 zilipinduka na nyingine 4 kuacha njia na kupelekea majeruhi 5 na kifo cha mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 7 aliyefahamika kwa jina la Hassan Lugano.
.
Aidha, Shirika hilo limesema kuwa linaendelea kufuatilia ili kufahamu chanzo cha ajali.