Polisi nchini Kenya inamsaka kijana wa miaka 20 Michael Muchiri aliyemuua babake mzazi John Mwangi na kuuteketeza mwili huo kwa mafuta ya petroli huku chanzo kikitajwa kuwa ni mzozo uliokuwepo baina yao.
Taarifa za awali zinasema kijana huyo alikuwa mrahibu wa dawa za kulevya kwa muda mrefu.
Polisi nchini Kenya wanasema sio mara ya kwanza kwa kijana huyo kuwashambulia jamaa zake huku ikidaiwa kuwa majuma yaliyopita alikuwa ametishia kumkatakata mamake mzazi na mama yake huyo aliokolewa na wanakijiji.