Back to top

RAIS SAMIA AWATAKIA KILA LA KHERI KIDATO CHA SITA

06 May 2024
Share

Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amewatakia kila la kheri wanafunzi wote wa Kidato cha Sita wanaoanza mitihani yao leo ya kuhitimu elimu ya sekondari leo na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awafanikishe katika hatua hiyo kwa mafanikio na kila jema katika hatua zinazofuata.

Taarifa ya Rais Samia ameipakia kwenye ukurasa wake wa Instagra na kusema anamani kuwa wanafunzi hao watakuwa wametumia muda wao shuleni kujiandaa vyema, hasa baada ya Serikali kuamua kufuta ada kwa Kidato cha Kwanza hadi cha Sita, kujenga na kuboresha shule zaidi, ujenzi wa mabweni sehemu ambazo wanafunzi, hasa wa kike, walikuwa kwenye mazingira hatarishi na kuongeza Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia uamuzi ambao umeleta nafuu na faraja katika familia nyingi na ongezeko la watahiniwa zaidi kutoka 106,883 mwaka Jana hadi 113,504 mnaoanza mitihani ya leo.