Back to top

BIL 5.7 KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU SONGWE

06 May 2024
Share

Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya kutatua changamoto na kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja mkoani Songwe ambayo yameharibiwa na mvua kubwa za El- nino zinazoendelea kunyesha Mkoani Songwe. 


Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga  baada ya kukagua sehemu zilizoathirika na mvua za El-Nino wilayani Songwe na Ileje.

Amesema kuwa Wilayani Songwe miundombinu imeharibika katika barabara ya Galula – Namkukwe sehemu ya Malangali, daraja la Mpona maji yalifurika juu na kukata mawasiliano kati Kijiji cha Namkukwe na Mpona.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo ameipongeza timu ya  wataalamu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kufanya kazi kwa haraka na ufanisi mkubwa kuhakikisha barabara zinapitika mkoani Songwe.


Sehemu nyingine ni Magamba eneo linalounganisha Kijiji cha Mpona na Igalula ambako sasa hivi linajengwa daraja na kuinua tuta la barabara, pia kwenye barabara ya Chang’ombe - Mkwajuni eneo la Zira miaka ya nyuma lilikuwa korofi; lakini mwaka huu halijapata changamoto kwa sababu Serikali kupitia TANROADS ilichukua hatua za mapema kulifanyia matengenezo.