
Rais Mteule ya Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Nane wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Hafla ya ku muapisha Rais Mteule Hussein Ali Mwinyi aliyezaliwa Disemba 23, 1966, imefanyika katika uwanja wa Amani mjini Unguja na kuhudhuriwa na vion gozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa.
Wengine ni Marais wastaafu Alhajj Ali Hassan Mwinyi wa awamu ya Pili na Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete wa awamu ya nne, Aman Abeid Karume, Makamu wa Rais Mstaafu Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, viongozi mbalimbali wa serikali zote mbili, mabalozi kadhaa pamoja na wananchi.
Matukio yaliyotangulia Kabla ya kiapo kilichoongozwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu ni pamoja na Rais Dkt.Ali Mohamed Shein kupigiwa mizinga ishirini na baadaye kukagua gwaride lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama Zanzibar na kisha bendera ya Rais anayemaliza muda iliteremshwa.
Baada ya tukio ndipo kilipofuata kiapo kilichoongwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu.
Baada ya kiapo ilifuata mizinga ishirini na mmoja iliyopigwa, tukio lililoambatana na wimbo wa taifa la Zanzibar na kupandishwa kwa bendera ya Zanzibar, kwa heshima ya Rais anayeingia madarakani na kisha zilifuata dua kutoka kwa viongozi wa dini.
Dua hizo zilifuatiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi alikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Zanzibar.
Marais waliomtangulia ni Sheikh Abeid Amani Karume, Skeikh Mminyi Aboud Jumbe, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Idris Abdul Wakil, Salmin Amour, Amani Abeid Karume na Dkt.Ali Hassan Mwinyi.
Akizungumza baada ya kuapishwa, Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka Wazanzibari waachene na tofauti zao bali washirikiane kuijenga Zanzibar mpya.
Aidha amewashukuru Wanzibari wote, wanaxchama wenzake wa Chama Cha Mapinduzi kwa kumuamini na kumpa heshima ya kuwaongoza na kuahidi kuwa atashirikiana na viongozi atakaowateua kutekeleza mipango yote ya maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Amevishukuru vyama vya upinzani vilivyoshiriki katika kinyanganyiro cha Urais wa Zanzibar ambavyo vimeahidi kushirikiana na serikali atakayoiunda katika kuijenga Zanzibar.
Leo ni siku ya mapumziko Zanzibar.