Back to top

Ndege ya jeshi ya Iran yaanguka,15 wasadikiwa kufa.

14 January 2019
Share

Watu 15 wasadikiwa kufa baada ya ndege ya mizigo ya jeshi la Iran Boeing 707 kuanguka  Mashariki mwa mji wa Tehran nchini Iran na baadaye kuteketea kwa moto.
 
Mkuu wa kitengo cha kupambana na majanga nchini humo Pir Hossein Koolivand  amesema kitengo chake hakina taarifa za undani kuhusiana na ajali hiyo.
 
Vyanzo vingine vya habari nchini humo vimesema ndege hiyo ilikuwa na watu zaidi ya kumi na wote wamekufa katika ajali hiyo.
 
Picha za kituo cha luninga cha nchi hiyo ya Iran zimekuwa zikionyesha moto ambao unawaka kutoka eneo ambalo ndege hiyo imeangukia.