
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetakiwa kuongeza ubunifu kwa kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge na mfuko huo na kwamba utakapokuwa na wanachama wengi wanaochangia, itasaidia mfuko huo kuwa endelevu.
.
Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo, Jijini Dodoma baada ya kupokea taarifa ya hali ya utendaji na majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
.
Mhe. Nyongo amesema kuna haja kubwa ya kusogeza elimu kwa wananchi waliopo ngazi za chini ili kuwa na uelewa juu ya umuhimu wa bima ya afya kabla ya kuanza kutekeleza sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
