Back to top

Nyati avamia Kijiji,aua mmoja na kujeruhi mmoja,Tanga

15 August 2019
Share

Mtu mmoja amefariki dunia huku mmoja akijeruhiwa vibaya baada ya kuvamiwa na Nyati wilayani kilindi mkoani Tanga

Akiongea na ITV majeruhi huyo ambae amelazwa katika  hospitali ya wilaya ya Handeni, amesema kuwa walikuwa wanaenda kuchota maji ghafla wakamkuta mnyama huyo aina ya Nyati ambae anae alikuwa anakunywa maji na ndipo alipoanza kuwakibimbiza na kusababisha maafa hayo. 

Mganga mkuu wa hospitali ya mji amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo na kwasasa amesema anaendelea vizuri.