Back to top

Ongezeko la maji Bwawa la Mtera wananchi watahadharishwa.

20 February 2021
Share

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limewatahadharisha wananchi wa vijiji vilivyopo kandokando mwa bwawa la Mtera na Kidatu ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, uvuvi na makazi kuwepo kwa ongezeko kubwa la maji kwenye bwawa la Mtera hivyo shirika hilo kulazimika kuyafungulia maji hayo yaliyohifadhiwa kwenye bwawa hilo.


Wakizungumza katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera kilichopo mpakani mwa Iringa Na Dodoma uongozi wa TANESCO umesema wanalazimika kufanya hivyo kutokana na bwawa hilo kujaa maji kupita kiasi ambapo wasipofanya hivyo kutaathiri uzalishaji wa umeme katika vituo hivyo.
.
Aidha, baadhi ya wakazi wanao tegemea bwawa hilo katika shughuli zao za kiuchumi wamebainisha kuwa tukio kama hilo limewahi kufanyika miaka ya nyuma na kuwaathiri kiuchumi.